Home Simba SC DILI LA KIUNGO MCONGO WA SIMBA LASHINDWA KUKAMILIKA

DILI LA KIUNGO MCONGO WA SIMBA LASHINDWA KUKAMILIKA

 DILI la kiungo, Doxa Gikanji raia wa Congo limekufa, kwa mujibu wa CEO wa Simba, Barbara Gonzalez.

Barbara amesema kuwa kilichokwamisha dili hilo ni ITC yake ambayo haitoweza kupatikana kwa wakati kwa sababu timu yake ya taifa ya Congo imefuzu hatua ya robo fainali ya CHAN. 

Ili kuipata ITC kabla ya dirisha la CAF kufungwa Januari 31 maana yake ni kumwondoa mchezaji huyo kwenye michuano ya CHAN.

Usajili wa Doxa ulizua maswali siku chache zilizopita baada ya jina lake kuonekana kwenye mfumo wa wachezaji waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya Ligi kuu Tanzania Bara na ilionekana kuwa raia wa Tanzania (Baadae TFF walitoa taarifa kwamba matatizo kama hayo hutokana na timu nyingi kuingiza majina dakika za mwisho).

Barbara amesema :”Timu ya Congo ipo hatua ya robo fainali Kwenye mihuano ya Chan nchini Cameroon ikiwa tutahitaji ITC yake ina maana kwamba hatakuwa na sifa kushiriki Chan,”.

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SABABU YA KUITUNGUA AL AHLY YA MISRI