Home epl BEKI WA ROMA YUPO SOKONI, UNITED NA CHELSEA ZAWANIA SAINI YAKE

BEKI WA ROMA YUPO SOKONI, UNITED NA CHELSEA ZAWANIA SAINI YAKE


GIANLUCA Mancini, beki wa Klabu ya Roma inaelezwa kuwa saini yake inawaniwa na timu kubwa mbili ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ambazo ni Manchester United na Chelsea.

Beki huyo mwenye miaka 24 amekuwa na msaada mkubwa ndani ya timu hiyo inayoshiriki Seria A na ameweza kutimiza majukumu yake kwa kuilinda timu hiyo kucheza mechi saba bila kufungwa na ametupia mabao manne.

Kwa mujibu wa The Express timu hizo ambazo zinashiriki Ligi Kuu England zipo tayari kumlipa nyota huyo mkwanja mrefu ili ziweze kupata huduma yake.

Ushindi wa Roma 3-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk ndani ya Europa League katika hatua ya 16 bora umedhihirisha uwezo wa nyota huyo ambaye dau lake linatajwa kuwa pauni milioni 27 na hii inatokana na janga la Virusi vya Corona.

Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjaer anatajwa kuweka mpango wa kuisaka saini yake ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chake ambacho kipo kwenye mazungumzo na nyota wao Eric Bailly ili kuongeza mkataba mpya.

Pia Solskjaer anahitaji kumuongezea mkataba beki wao wa kati Harry Maguire, United inatajwa kuingia kwenye rada za kuisaka saini ya nyota wa RB Leipzing, Ibrahim Konate na Jules Kounde wa Sevilla.

SOMA NA HII  RONALDO AFIKISHA JUMLA YA HAT TRICK 58