Home Yanga SC WACHEZAJI WAWILI WA KIKOSI CHA KWANZA WAONDOKA YANGA

WACHEZAJI WAWILI WA KIKOSI CHA KWANZA WAONDOKA YANGA

 


TONOMBE Mukoko raia wa Congo pamoja na Haruna Niyonzima wa Rwanda ambao wote ni viungo washambuliaji wameondoka ndani ya kikosi hicho na kuelekea nchini kwao kwa ajili ya kujiunga na timu zao za Taifa.


Mukoko ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea Klabu ya AS Vita yeye ameitwa kwa mara ya kwanza ndani ya timu ya taifa ya Congo tangu kuijiunga na Klabu ya Yanga ikiwa ni kwa ajili ya kufuzu michuano ya AFCON.

Niyonzima yeye ni mzoefu na amekuwa akiitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda.
Viungo hao wawili kwa sasa wote wana uhakika wa namba kikosi cha kwanza ambapo Niyonzima zama za Cedric Kaze alikuwa hapati nafasi ya kuanza licha ya kwamba alipewa jukumu la kuwa nahodha kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup.
Akiwa visiwani Zanzibar, Niyonzima alikiongoza kikosi hicho kusepa na taji la Mapinduzi na kuwa ni la kwanza na la mwisho kwa Kaze kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa amechimbishwa Machi 7 baada ya timu kuwa kwenye mwendo wa kusuasua mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  MWAMBUSI ATANGAZA PANGA, PANGUA YANGA