Home Uncategorized LIPULI YATAJA INACHOKITAKA LIGI KUU MSIMU UJAO

LIPULI YATAJA INACHOKITAKA LIGI KUU MSIMU UJAO


UONGOZI wa Lipuli umesema kuwa msimu ujao hauna hesabu ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara wao hesabu zao ni kushika nafasi tano za juu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Lipuli  Clement Sanga amesema kuwa malengo makubwa ni kuwa ndani ya nafasi tano za juu

“Tumejipanga na kipaumbele chetu kikubwa ni kuona kwamba tunashika nafasi tano za juu hasa ile nafasi ya pili na ya tatu hatuna mpango wa kutwaa ubingwa.

“Vijana wanajiweka fiti kuelekea Agosti 23 ambapo ligi inatarajiwa kuanza na kila kitu kipo sawa mashabiki watupe sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA JUMAPILI