Home Uncategorized NIYONZIMA ATUMA UJUMBE KWA KMC LEO

NIYONZIMA ATUMA UJUMBE KWA KMC LEO

HARUNA Niyonzima, kiungo myumbulifu ambaye amechezea timu za Simba na Yanga amesema kuwa leo kazi ni moja tu kutafuta ushindi mbele ya KMC.

KMC leo itatupa karata yao ya kwanza kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Kigali kwenye kombe a Shirikisho Afrika kabla ya kureajeana na wapinzani wao kati ya Agosti 23-25.

Niyonzima kwa sasa ni mali ya AS Kigali baada ya kumalizana na Simba amesema watapambana kupata matokeo.

“Ni mchezo mgumu kwetu na ninatambua kwamba KMC ni moja ya timu bora kwenye ligi ya Bongo ila hilo halitupi mashaka kwani nasi pia tupo vizuri tutaonyesha kitu cha kipekee,” amesema kiungo huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba.

SOMA NA HII  LIGT AUNGANA NA CR7 JUVENTUS, ASAINI MIAKA MITANO