Home Habari za michezo KISA CAF….MASTAA YANGA WAGAWANYWA KILAZIMA….”LAZIMA UPANDE UUMIE”…

KISA CAF….MASTAA YANGA WAGAWANYWA KILAZIMA….”LAZIMA UPANDE UUMIE”…

Habari za Yanga leo

Wakati Fainali za Mataifa Afrika zikifikia hatua ya 16 bora ratiba imewagonganisha mastaa wawili wa Ligi Kuu Bara ambao watajikuta wanapunguzana wenyewe.

Baada ya Taifa Stars kuishia tena hatua ya makundi macho ya mashabiki wengi hususan nashabiki wa Yanga watajituliza Januari 30 kwenye mchezo wa mwisho wakiwatazama mastaa wao kipa namba moja wa Mali Djigui Diarra atakapokuwa vitani na kiungo wake Stephanie Aziz KI.

Mechi hiyo itakayoanza saa 2:00 usiku itawakutanisha mastaa hao wa Yanga ambao watalazimika kuwa maadui kwa dakika 90-120 kila mmoja akitetea bendera ya timu yake.

Mshindi wa mchezo huowa Diara na Mali yake dhidi ya Aziz KI na Burkina Faso atakwenda robo fainali kukutana na mshindi wa mchezo kati ya bingwa mtetezi Senegal atakayekutana na mwenyeji Ivory Coast Januari 29 saa 5:00 usiku.

Achana na Diara Simba wao watakuwa na utulivu wakimtazama staa wao beki Henock Inonga akiwa na taifa lake DR Congo Januari 28 saa 5:00 usiku atakapokuwa na vita ya soka dhidi ya Misri isiyotabirika.

Endapo Congo itafuzu hatua hiyo mbele ya Misri itakwenda robo fainali kukutana na mshindi wa mchezo wa majirani kati ya Guinea ya Ikweta dhidi ya Guinea Bissau mechi ambayo itapigwa Januari 28 saa 2:00 usiku.

Mechi zingine za hatua hiyo ya 16 bora ni pamoja na Angola dhidi ya Namibia watakaokutana Januari 27 saa 2:00 usiku, kisha baadaye saa 5:00 usiku Nigeria watapambana na Cameroon.

Cape Verde wao watakutana na Mauritania Januari 29 saa 2:00 huku Morocco wakikutana na Afrika Kusini januari 30 saa 5:00 usiku.

SOMA NA HII  SIMBA INAZIDI KUJICHIMBIA KABURI LIGI KUU