Home Habari za michezo SIMBA INAZIDI KUJICHIMBIA KABURI LIGI KUU

SIMBA INAZIDI KUJICHIMBIA KABURI LIGI KUU

Habari za Simba

SIMBA inazidi kujiweka kwenye mazingira magumu ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na KMC kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Sare hiyo imeifanya Simba iendelee kukaa nafasi ya tatu kwenye msimamo nyuma ya Azam na Yanga.
KMC ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 31 kupitia kwa staa wake Waziri Junior ambaye alipata pasi kutoka kwa Awesu Awesu aliyeuanza mpira wa adhabu ndogo haraka na kumpasia mfungaji.
Dakika ya 57, Simba ilisawazisha kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Said Ntibazonkiza likiwa ni bao lake la tatu kwa mkwaju wa penalti kati ya manne ambayo amefunga kwenye ligi msimu huu.
Iliichukua Simba dakika moja kupata bao la pili katika dakika ya 58, lililofungwa Jean Baleke aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya John Bocco.
Dakika ya 89, KMC ilisawazisha kupitia tena kwa Junior aliyetumia vyema makosa ya kipa wa Simba, Ayoub Lakred aliyeutema mpira uliopigwa na winga Tepsi Evans, likiwa ni bao lake la saba kwenye ligi msimu huu.
Katika mechi 10, Simba imeshinda saba, sare mbili, imefungwa mchezo mmoja ina pointi 23, inashika nafasi ya tatu, Yanga 27 michezo 10, Azam FC pointi 31 michezo 13.
Mechi za Simba KMC
19/12/2018- Simba 2-1 KMC
25/4/2019- KMC 1-2 Simba
28/12/2019- KMC 0-2 Simba
1/3/2020- Simba 2-0 KMC
16/12/2020- Simba 1-0 KMC
7/7/2021- KMC 0-2 Simba
24/12/2021- KMC 1-4 Simba
19/7/2022- Simba 3-1 KMC
7/9/2022- Simba 2-2 KMC
26/12/2022- KMC 1-3 Simba
23/12/2023- KMC 2-2 Simba.
Zimekutana mara 12, ambapo Simba imeshinda michezo 9 na kutoka sare mitatu.
Kwa maana hiyo tangu KMC ipande Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/2019, haijawahi kuifunga Simba.

SOMA NA HII  YANGA ISIWACHUKULIE POA AL AHLY