Home Habari za michezo YANGA SIO KINYONGE….. WAFUNGA MWAKA KWA MTINDO HUU

YANGA SIO KINYONGE….. WAFUNGA MWAKA KWA MTINDO HUU

Meridianbet

BINGWA mtetezi Yanga bado anaendelea na safari yake akitaka kutetea taji lake la tatu mfululizo la Ligi Kuu Bara baada ya kushinda mchezo wake mwingine ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Tabora United na ikiwa ni sawa na kuwaambia mashabiki wao Tukutane mwakani.

Bao la mpira wa adhabu la kiungo wake mshambuliaji Stephanie Aziz KI likatosha kuipa Yanga ushindi huo muhimu uliowabakisha nafasi ya pili ikiendelea kuitafuta Azam inayoongoza ligi lakini ikiwa mbele yao kwa michezo miwili.

Aziz KI alifunga bao hilo kwa shuti kali lililojaa moja kwa moja wavuni nje kidogo ya eneo la hatari ambapo kipa wa Tabora, John Noble atajilaumu kwa hesabu zake wakati akitaka kuokoa shuti hilo akiwa amesogewa mbele kidogo ya lango na mfungaji kumchungulia vizuri.

Bao hilo linakuwa la 10 kwa Aziz KI sawa na namba ya jezi yake mgongoni akiendelea kuongoza msimamo wa ufungaji bora akiendelea kuwakimbia wenzake.

Yanga hata hivyo haikuwa na na ushindi rahisi mbele ya Tabora ambao ilionekana kutulia na kupeleka mashambulizi lango la wageni lakini umakini wao ulikuwa mdogo kuweza kumalizia.

SOMA NA HII  SAMATTA: NI BAHATI MBAYA TUNAANZIA UGENINI...NIGER NAO WANAITAMAN AFCON KAMA SISI...