Home Habari za michezo HAO YANGA vs SINGIDA VIKOSI VYAO LEO SIO POA

HAO YANGA vs SINGIDA VIKOSI VYAO LEO SIO POA

Geita vs Yanga

Kwa vikosi na takwimu zilivyo leo lazima mtu aseme sana kwenye Uwanja wa Mkapa, Yanga itakavyowakabisha Singida kwenye mechi ya Ligi. Dakika 90 za leo kuanzia saa 12:15 jioni, zitakuwa na majibu mengi.

Kuonyesha kuwa ni siku ya kuviziana muda mchache baada ya mechi hii kumalizika, Azam watakuwa kwenye Uwanja wa Azam Complex saa 2:30 usiku kuvaana na KMC kwenye mchezo mwingine wa kibabe.

Yanga wanakwenda kwenye mchezo huu ikiwa kinara katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 15 huku Singida ikiwa na pointi nane kwenye michezo sita katika nafasi ya sita hadi sasa, ikiwa inatakiwa kushinda mchezo huu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.

Katika michezo miwili ya Ligi Kuu ambayo wamekutana huko nyuma, Singida imepoteza yote jambo ambalo linawapa kiburi mashabiki wa Yanga kuamini kuwa hata wa leo wanaweza kuibuka na ushindi kama walivyofanya kwa Azam.

USHINDI MUHIMU

Yanga ina pointi 15 sawa na Simba, lakini yenyewe ikiwa na mchezo mmoja zaidi, hivyo ili waendelee kutamba mjini wikiendi hii ushindi ni muhimu kufikisha pointi 18, hali ambayo itawalazimu Simba nao kushinda kesho ili wakimbizane kileleni.

UTAMU ULIPO

Yanga wanatengemea tena makali ya kiungo wao mahiri, Stephen Aziz Ki, ambaye hadi sasa ndiye kinara wa mabao kwenye ligi akiwa ameshafunga mara sita, moja mbele ya mshambuliaji wa Simba Jean Baleke mwenye matano.

Kama Ki, atafunga tena mabao matatu leo kama alivyofanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Azam, atakuwa ameweka rekodi mpya kwake ya kufikia idadi ya mabao ambayo alifunga kwenye ligi msimu mzima uliopita, ambao alifunga mara tisa.

Hata hivyo, atakutana na kigingi cha mabeki wa Singida ambao wameonyesha kiwango kizuri hadi sasa wakiruhusu nyavu zao kuguswa mara sita tu katika michezo sita, ukiwa ni wastani wa bao moja kwenye kila mchezo.

YAO NA TCHAKEI

Katika mchezo dhidi ya Azam, Yanga walikosa huduma ya beki wao mahiri kwa sasa, Yao Kouassi, ambaye alikuwa majruhi.

Anaongoza kwa pasi tatu za mabao, lakini pamoja na uwepo wake yeye pamoja na mabeki wenzake watakuwa na kibarua cha kumzuia, mshambuliaji Marouf Tchakei raia wa Togo, ambaye amekuwa mwiba kwa sasa akiwa ameshapachika mabao matatu.

Makocha

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema mchezo wao dhidi ya Singida BS utakuwa mzuri na mgumu kutokana na namna ambavyo walivyo wapinzani wao.

Gamondi alisema jambo kubwa ambalo anajivunia ni sifa na uwezo wa wachezaji wake akiamini kabisa watakwenda kupambana kibabe. “Tumecheza mechi wiki hii na kuna muda wachezaji wanakuwa hawapati muda mzuri wa kupumzika lakini kama kocha kuna maamuzi tunayafanya na mtaona wachezaji 11 watakaoanza.

“Singida ni timu nzuri na nimeona kwenye mashindano ya Caf namna inavyocheza na hata kwenye ligi, napenda mechi za namna hii kwa sababu zinateka hisia za mashabiki,” alisema Gamondi ambaye ni raia wa Argentina.

Kocha msaidizi wa Singida BS, Thabo Senong alisema kila kitu kilishamalizika upande wa maandalizi kwa ajili ya mchezo huu kuhakikisha wanapata pointi tatu.

Senong alisema wanawaheshimu wapinzani wao lakini wanajivunia kuwa na wachezaji ambao wanaweza kubadili matokeo muda wowote.

“Sote sisi mechi zetu za mwisho tumetoka kushinda kwa hiyo kuna hali ambayo tunayo, kikubwa ni kwenda kupambana ndani ya uwanja.

“Timu yoyote ambayo itafanya makosa mengi itapoteza mchezo, timu itakayofanya makosa machache itatoka na ushindi.”

SOMA NA HII  BENZEMA AHUSISHWA NA UGAIDI KUFUATIA SAKATA PALESTINA