Home Habari za michezo GAMONDI AFANYA MAAMUZI HAYA MAMBO YAISHE

GAMONDI AFANYA MAAMUZI HAYA MAMBO YAISHE

Habari za Yanga leo

Baada ya timu yake kupoteza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Angel Gamondi amesema sababu kuu ya kuziacha Pointi zote tatu ugenini, ni safu yake ya ulinzi kufanya makosa ambayo wenyeji Ihefu SC waliyatumia vizuri.

Ihefu FC ilifanikiwa kuifunga tena Young Africans mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Highland Estates ulioko Mbarali, Mbeya na kufikisha Pointi sita.

Gamondi amesema wapinzani wao walitumia makosa hayo machache huku wachezaji wake wakishindwa kuzitumia vyema nafasi walizozitengeneza na hivyo kulala katika mchezo huo na si kwa sababu ya mwamuzi.

Gamondi amesema licha ya mwamuzi wa mchezo huo kutotenda haki kutokana na baadhi ya maamuzi yake kuwaumiza mabingwa hao watetezi wakati wakielekea kufanya mashambulizi.

“Hali hiyo imekatisha tamaa kwa wachezaji wangu, hatuwezi kuwatupia lawama waamuzi kwa sababu walifanya majukumu yao na wachezaji walishindwa kutumia nafasi walizozitengeneza ili kufunga.”

“Kulitokea changamoto nyingi katika mechi ya juz), wengine wamepoteza muda lakini mwamuzi alikuwa na jukumu la kuzuia hayo, hatukuweza kusema tumefungwa kwa ajili ya makosa yake, tunapaswa kuchukuwa lawama za kupoteza mchezo huu.” amesema Gamondi.

Kocha huyo amesema alifanya mabadiliko mengi katika mechi hiyo lakini kipindi chote cha kwanza walicheza vizuri na kosa ililofanywa na kipa wao, Djigui Diarra ni la kawaida katika mpira.

Ameongeza wachezaji wake hawakuonyesha kiwango kizuri katika kipindi cha pili hivyo liwafanya wenyeji kuendelea kutawala mechi hiyo.

Mechi hii imemalizika, ninawataka wote wasahau matokeo na kujipanga kuelekea mechi yao ijayo, tunakwenda kurekebisha makosa na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo mwingine ambao tutaenda ugenini,” ameongeza Kocha huyo kutoka nchini Argentina

Tayari Young Africans imeshawasili jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko watano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold utakaopigwa kesho Jumamosi (Oktoba 07), Uwanja wa CCM Kirumba.

SOMA NA HII  MWAKALEBELA: NINABEBESHWA MIZIGO ISIYONIHUSU