Home Uncategorized MWAKALEBELA: NINABEBESHWA MIZIGO ISIYONIHUSU

MWAKALEBELA: NINABEBESHWA MIZIGO ISIYONIHUSU


FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa ikiwa kuna jambo baya ambalo amelifanya ndani ya Yanga wamwambie kwa sasa kwa kuwa anabebesha mizigo isiyomuhusu kila wakati.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba miongoni mwa viongozi ambao wanaihujumu Yanga ni pamoja naye jambo ambalo limemfanya asiwe na furaha.

Mwakalebela amesema:”Nimekuwa nikiambiwa kwamba ninafanya mambo ambayo sio sawa na mambo yote mabaya ninaambiwa ni mimi katika hili mimi sina furaha kwa kweli.

“Kila baya la Yanga ninatajwa mimi, kwani nina nguvu gani ndani ya Yanga ya kuweza kufanya yote hayo? Ikiwa kuna jambo ambalo wanahitaji nifanye basi waniambie kwa sasa kwani sio sawa kupeana mizigo ambayo haina ukweli,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI