Home CAF HATIMA YA TANZANIA KUANDAA AFCON 2027 KUJULIKANA WIKI IJAYO…

HATIMA YA TANZANIA KUANDAA AFCON 2027 KUJULIKANA WIKI IJAYO…

Habari za Michezo leo

Hatma ya maombi ya Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) itajulikana Jumatano (Septemba 27) katika mkutano utakaofanyika jijini Cairo, Misri kwa wajumbe kupiga kura.

Tanzania, Kenya na Uganda ziliwasilisha maombi ya pamoja na jana viongozi wake walikutana Dar es salaam ili kupanga mikakati.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakubu alisema wameandaa mikakati imara ya kuhakikisha wanapata wenyeji ikiwamo kwenda kufanya kampeni za pamoja kwa njia za kidiplomasia.

“Makatibu wakuu wa wizara za michezo, kutoka nchini zetu tatu za Kenya, Uganda na Tanzania tulikutana, na tayari tumepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), inayoeleza Septemba 27, mwaka huu ndio kura ya kuamua nani awe mwenyeji wa fainali hizo zitapigwa huko Cairo, kwa hiyo tuliona nchi zetu tulizoomba kwa pamoja tukutane tupange mikakati namna ya kupata ushindi, ” Yakubu alisema.

Alisema baada ya hapo kulitarajiwa pia kuwa na kikao cha Mawaziri wa Michezo wa nchi hizo.

Alisema wanajipanga kwenda Misri kwa ajili ya kufanya kampeni ambazo zitakuwa na lengo la kuwashawishi wajumbe wawapigie kura kwa sababu kuna nchi nyingine zimeomba kuandaa fainali hizo.

“Kikubwa ambacho CAF wanataka kuangalia ni miundombinu ambapo kwa sisi hatuna shaka nalo, tunaendelea na maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa na pia tunatarajia kujenga viwanja vingine, tutatumia viongozi wenyeu shawishi kama njia za kidiplomasia pamoja na kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia pamnoja na Leodegar Tenga, ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa CAF, natumai juma lijalo tutakuwa na habari njema, tuombeane heri,” alisema kiongozi huyo.

Kama maombi hayo yatafanikiwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki iliyo chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan, Yoweri Museveni (Uganda) na William Ruto wa Kenya kuweka historia.

SOMA NA HII  DIARRA YANGA MAMBO YAZIDI KUNOGA, ALAMBA DILI HILI LA KIBABE