Home Habari za michezo KWA HILI LA MIQUISSONE NA NTIBAZONKIZA….IPO SIKU SIMBA ‘KITANUKA’….

KWA HILI LA MIQUISSONE NA NTIBAZONKIZA….IPO SIKU SIMBA ‘KITANUKA’….

Habari za Simba SC

Viungo wawili wa Simba, Luis Miquissone na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kuna namna wanazidi kuiva chungu kimoja kutokana na muunganiko wao kuanza kujibu.

Nyota hao kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 6, mwaka huu, mpira wa kona uliopigwa na Luis dakika ya 74, uleleta bao la pili.

Katika mchezo huo, Luis alipiga kona kwa kumpa pasi Saido ambaye alijaza krosi iliyokutana na Fabrice Ngoma aliyepachika bao la pili dakika ya 75 kwa pigo la kichwa.

Ngoma ilijibu kwa mara nyingine kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos uliochezwa Zambia, mpira wa kurushwa wa Saido ulikutana na Luis aliyempa pasi ya bao Chama.

Chama alipachika bao hilo la pili dakika ya 90 na ubao ukasoma Power Dynamos 2-2 Simba. Katika mechi walizocheza dhidi ya Power Dynamos mapigo yao yalijibu.

SOMA NA HII  SALAMBA AFUNGUKA A-Z KINACHOMPA MADILI YA KUCHEZA KWA WAARABU...AITAJA SIMBA ....