Home Habari za michezo RAIS ATOA TAMKO HILI ZITO YANGA…BENCHI LA UFUNDI LATAJWA…AMEZUNGUMZA HAYA

RAIS ATOA TAMKO HILI ZITO YANGA…BENCHI LA UFUNDI LATAJWA…AMEZUNGUMZA HAYA

MECHI HII YA YANGA YAPELEKWA MBELE...HUYO NABI SASA!!

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa tayari umeshazungumza na wachezaji wao juu ya kuuheshimu mchezo wao wa marudiano dhidi ya Rivers United licha ya kuibuka na matokeo ya ugenini dhidi ya Rivers United.

Yanga kwa sasa wanafurahia matokeo waliyoyapata ugenini dhidi ya Rivers ya mabao 2-0 jambo ambalo linawafanya kutanguliza mguu mmoja kuelekea hatua inayofuata ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza nasi, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alisema kuwa tayari benchi la ufundi na uongozi wameshazungumza na wachezaji juu ya umuhimu wa mchezo huo na wasione kuwa tayari
wameshamaliza baada ya kupata ushindi katika mchezo wa kwanza kule Nigeria.

“Benchi la ufundi pamoja na viongozi tayari tumeshazungumza na wachezaji juu ya kuwaeleza umuhimu wa huu mchezo na wasione kuwa tayari wameshamaliza kazi kwani kuna mchezo wa marudiano huu wa hapa nyumbani kwetu.

“Hivyo ambacho tunachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha kuwa tunapambania matokeo yetu kwa kucheza kwa kujituma kama kawaida kuhakikisha kuwa tunashinda mechi hii na tuweze kuandika historia nyingine mpya,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA IBENGE KUTUA AZAM FC....AL HILAL WATOA TAMKO RASMI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here