Home Simba SC MORRISON: KWA SIMBA HII, MTASUBIRI MIAKA 20 HADI 30

MORRISON: KWA SIMBA HII, MTASUBIRI MIAKA 20 HADI 30

 


KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba, Bernard Morrison amefunguka kuwa ana imani kubwa klabu yake itaendelea kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka 15 hadi 20 ijayo.

Nyota huyo mwenye uraia wa Ghana alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho jana kiliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini, katika robo fainali ya pili ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Licha ya ushindi huo Simba ilishindwa kusonga mbele kutokana na tofauti ya bao moja baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Afrika Kusini.

Baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo Morrison amesema: “Ninajivunia sana kuvaa jezi hii ya Simba, tumetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini tunajipanga kuhakikisha tunashinda makombe yote yaliyobaki. Simba itaiwakilisha Tanzania kwa miaka 15 Hadi 20 ijayo,”

SOMA NA HII  AL HILAL YAWASILI BONGO,SABABU ZA SIMBA SUPER CUP ZAWEKWA WAZI