Home epl GUNDOGAN: HAVERTS NI MCHEZAJI BORA ANA VITU VYA KIPEKEE

GUNDOGAN: HAVERTS NI MCHEZAJI BORA ANA VITU VYA KIPEKEE


IIKAYA Gundogan nyota wa kikosi cha Manchester City amesema kuwa anaamini kwamba kiungo wa Klabu ya Chelsea, Kai Haverts ana ubora licha ya kupata ugumu ndani ya kikosi hicho.

Gundogan ambaye pia ni nyota katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani amesema kuwa mchezaji huyo ni kati ya wale wenye mbinu za kipekee wawapo uwanjani.


Harvets na Gundogan wapo pamoja kwenye timu ya taifa ya Ujerumani jambo ambalo linawafanya wawaweze kuwa na ushkaji.

Gundogan amesema kuwa anaamini kwamba nyota huyo ambaye aliibuka ndani ya Chelsea akitokea Klabu ya Bayern Leverkusen ya Bundesliga atakuja kufanya vizuri hapo baadaye.

“Kai ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa ambao ni wa kipekee. Nafikiri ni mchezaji na bora kwa umri wake anaendelea kupambana,” .

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI WA ARSENAL, LACAZETTE AINGIA ANGA ZA BARCELONA