Home Uncategorized MASHABIKI WA MISRI BADO HAWAAMINI, MBIO ZA SALAH ZAFIKA UKINGONI

MASHABIKI WA MISRI BADO HAWAAMINI, MBIO ZA SALAH ZAFIKA UKINGONI


MOHAMED Salah mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Misri anayekipiga timu ya Liverpool kwa sasa naye atakuwa ni mtazamaji wa michuano ya Afcon ambayo inaendelea nchini Misri baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Timu ya Taifa ya Afrika Kusini.

Mashabiki wengi wa Misri bado hawaamini wanachokiona mbele yao kwamba nao wanabaki kuwa watazamaji kwani walibeba matumaini makubwa ya kushinda mwisho wa siku wakaambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzani wao Afrika Kusini.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Thembinkos Lorch dakika ya 85 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuifanya Afrika Kusini kutinga hatua ya robo fainali.

Mchezo mwingine ambao ulikuwa na ushindani ambao wataalamu na wachambuzi wa soka wanasema mpaka sasa hakuna mchezo kama huo uliochezwa ni ule kati ya Cameroon na Nigeria.

Dakika 90 zilikamilika kwa Nigeria kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 hivyo nao wanatinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo kwa sasa ushindani unazidi kunoga.

Mpaka sasa tayari, Senegal, Benini, Nigeria na Afrika Kusini zimetinga hatua ya robo fainali.

SOMA NA HII  NYOSSO KUKIPIGA NDANI YA RUVU SHOOTING