Home Uncategorized ZAHERA ALIAMSHA DUDE YANGA, AWAGOMEA MAKOCHA WAZAWA

ZAHERA ALIAMSHA DUDE YANGA, AWAGOMEA MAKOCHA WAZAWA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hatokuwa tayari kufanya kazi na kocha mzawa ambaye atatafutiwa na viongozi wa Yanga.

Zahera amesema ameskia taarifa za viongozi wa Yanga kuanza kufanya mchakato wa kumtafutia kocha msaidizi kwa ajili ya msimu ujao ambaye atakuwa mzawa jambo ambalo hakubaliani nalo.

“Najua kuna matatizo makubwa sana kufanya kazi na mzawa, haina maana kwamba hawezi kufanya kazi hapana ni matatizo tu ambayo wanayo hasa kwenye benchi la ufundi.

“Kocha mzawa sitafanya naye kazi, mimi ninamtafuta kocha wangu mwenyewe,” amesema Zahera.

SOMA NA HII  SAIDO NTIBANZOKIZA KUANZA NA DODOMA JIJI