Home Uncategorized AZAM KUIFUMUA YANGA, KMC

AZAM KUIFUMUA YANGA, KMC


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utamtangaza kocha wa kikosi hicho hivi karibuni huku akidokeza kuwa anatoka ndani ya Ligi ya bongo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Popat amesema ni suala la muda kwa kuwa mipango ipo sawa.

“Kila kitu kwa sasa kipo sawa na tutamtangaza kocha muda wowote hivi karibuni, anaweza kuwa wa KMC,(Etiene Ndiyaragije), ama yule wa Yanga,(Mwinyi Zahera) hata wa Simba (Patrick Aussems).

“Kuhusu kocha Idd Cheche yeye ataendelea kuwa kocha msaidizi na Abdul Mingange atarejea kwenye timu yake ya vijana kwa kuwa ndiko alikokuwa,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA NABI, MORISSON WATUPWA NJE YA DIMBA FAR RABAT HAWANA CHAO