Home Habari za michezo MCHAMBUZI AMPA USHAURI HUU ROBERTINHO LEO DHIDI YA AL AHLY

MCHAMBUZI AMPA USHAURI HUU ROBERTINHO LEO DHIDI YA AL AHLY

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Salama Ngale amesema kuwa safu ya kiungo ya Klabu ya Simba bado inapwaya hivyo kocha wao, Robertinho anapaswa afanye kazi ya ziada leo kuingia na mbinu mbadala ya kuwadhibiti Al Ahly.

Simba na Ahly watakuwa dimbani leo Ijumaa, Oktoba 2023 kumenyana na kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya African Football utakaopigwa majira ya saa 12:00 katika Dimba la Mkapa.

“Ngoma ni mchezaji mzuri na anapiga pasi nzuri ambazo zinakwenda kuleta madhara kubwa lengo la mpinzani.

“Robertinho amejaribu pacha ya Kanoute na Mzamiru bado inapwaya, lakini pacha ya safu ya ulinzi anayoikubali sana ni ya Ngoma na Mzamiru licha ya kwamba Ngoma bado hajawa katika kiwango chake kile.

“Kwangu mimi naona Robertinho kama ataanza na viungo wote watatu, Kanoute, Mzamiru pamoja na Ngoma ili kuipa nguvu zaidi safu ya ulinzi ukilinganisha na ubora wa viungo wa Al Ahly,” amesema Salama Ngale wa UFM.

SOMA NA HII  ZILE TAARIFA ZA MZEE DALALI KUPATA AJALI ZIKO HIVI...BODABODA KAKIMBIA...MWANAE KAITAJA SIMBA...