Home Uncategorized MUANGOLA HUYU AINGIA ANGA ZA YANGA

MUANGOLA HUYU AINGIA ANGA ZA YANGA

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga iko kwenye hatua za mwisho za  kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Interclube ya Angola, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes ‘ Carlinhos’ raia wa Angola.


Hiyo ni siku chacha baada ya kukamilisha dili la nyota wawili wa kimataifa kujiunga na timu hiyo kwa dili la miaka miwili ambao ni Tuisila Kisinda ambaye ni kiungo pamoja na Tonombe Mukoko ambaye yeye ni mshambuliaji.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa bado kuna nyota wengine wa kimataifa wanafanya nao mazungumzo hivyo mipango ikamilika wataweka kila kitu wazi.

“Kuna nyota mwingine raia wa Angola tupo naye kwenye mazungumzo ya mwisho, mambo yakikamilika basi kila kitu kitawekwa wazi,” amesema.
SOMA NA HII  KINDA WA BOUNRERMOUTH ATABIRIWA MAKUBWA MSIMU UJAO NDANI YA LIGI KUU ENGLAND