Home Uncategorized KMC YATEMBEZA PIRA SPANA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA DODOMA JIJI

KMC YATEMBEZA PIRA SPANA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA DODOMA JIJI

 


KLABU ya KMC leo Desemba 4 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


Ikiwa na sera ya pira spana, pira mapato ilitumia dakika 45 za mwanzo bila kugusa lango la mpinzani na kuzifanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.

Kipindi cha pili KMC iliongeza kasi ya mashambulizi ambayo ilileta matunda kwao kwa kuweza kutumia nafasi moja waliyoipata.

Bao pekee la ushindi kwa KMC lilifungwa  na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 58 baada wana Kino Boys kuliandama lango la Dodoma Jiji.


Mvuyekure alipachika bao hilo kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa kwa guu la kushoto na Ally Ramadhani.


Mvuyekure amesema kuwa maandalizi mazuri yamewapa matokeo na kusepa na pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  MCHAMBUZI AMPA USHAURI HUU ROBERTINHO LEO DHIDI YA AL AHLY