Home news HAJI MANARA AKWEA PIPA NA BOSI WAKE

HAJI MANARA AKWEA PIPA NA BOSI WAKE


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga leo Septemba 28 amekwea pipa kuelekea Kagera kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Bara kesho Uwanja wa Kaitaba. 


Mchezo huo ni wa ligi na utakuwa ni kwanza kwa Yanga kwa msimu mpya wa 2021/22 huku malengo makubwa yakiwa ni kwenye kusepa na pointi tatu muhimu.

Manara ameongozana na bosi wake mkubwa, Senzo Mbata ambaye ni Kaimu Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Yanga.

Ikumbukwe kwamba viongozi hawa wawili kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa ndani ya Simba, ambapo Manara alikuwa ni Ofisa Habari wa Simba na Mbatha alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa Simba.

Kesho timu ya Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar.


SOMA NA HII  VIDEO: MCHEZAJI BORA WA SIMBA QUEENS AWEKA WAZI MIPANGO IJAYO