Home news MANARA – YANGA TUMESITISHA SHEREHE…HATUTAKI KULALAMIKA LALAMIKA OVYO

MANARA – YANGA TUMESITISHA SHEREHE…HATUTAKI KULALAMIKA LALAMIKA OVYO


Wakati kikosi cha Yanga kikitua salama mkoani Kagera, Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema malengo makubwa kwao ni kuhakikisha wanachukua makombe yote ya ndani.

Manara ameyasema hayo jana akisema baada ya kushinda mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba wanasitisha furaha hiyo na kurudi haraka kujipanga na Ligi Kuuu Bara.

Yanga itafungua pazia la ligi Jumatano Septemba 29 wakikabiliana na wenyeji wao Kagera Sugar mchezo utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba.

Manara amesema baada ya kuifunga Simba kwa bao 1-0 wanataka kuanza ligi kwa kasi ili waweze kuweka hai malengo yao.

“Tumeshinda mechi kubwa ambayo kila mmoja ameona ubora wa timu yetu,nitangaze rasmi sisi kama viongozi tulishasitisha sherehe za ushindi huo,” amesema Manara.

“Tuna malengo makubwa msimu huu na yako wazi kuchukua mataji yote mawili ya ndani na tuna timu imara itakayoweza kufanikisha hilo.

” Tumetoka kupoteza nafasi ya mashindano ya Afrika soka lina matokeo hayo lakini sasa Yanga haiko tayari kuendelea kusotea mataji haya ya ndani.

Aidha Manara ameongeza kwamba Yanga inategemea uendeshaji bora wa ligi na sio kuendelea kwa kushamiri kwa changamoto zilizotokea msimu uliopita.

“Changamoto zote za uendeshaji wa ligi zilizotokea msimu uliopita zinajulikana na Yanga hatutaki kulalamika tuna timu imara lakini tunatarajia yale yote yaliyotokea yatakuwa yamefanyiwa kazi.”

SOMA NA HII  KISA KIPIGO KUTOKA COASTAL ....KASEJA AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA NAMNA ALIVYOCHEZA CHINI YA KIWANGO...