Home news HAWA HAPA SITA WA SIMBA KUIKOSA BIASHARA UNITED

HAWA HAPA SITA WA SIMBA KUIKOSA BIASHARA UNITED


 IMEELEZWA kuwa nyota sita wa Simba wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Karume, Mara.

Nyota hao ni Ibrahim Ajibu ambaye ni kiungo mshambuliaji, huyu ana matatizo ya kifamilia pamoja na Sadio Kanoute ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Mwingine ni beki wa kati, Joash Onyango ambaye aliumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kugongana na mchezaji mwenzake kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Kiungo mkongwe, Jonas Mkude huyu anatajwa kutokuwa sehemu ya kikosi na nyota mwingine ambaye ataukosa mchezo wa leo ni Bernard Morisson ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu hii ni mechi yake ya pili.

Hata Taddeo Lwanga ambaye ni kiungo atakosekana kwenye mchezo wa leo kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu ambayo alionyeshwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga baada ya kuonyeshwa kadi za njano mara mbili.

Kuhusu mchezo wa leo, Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema kuwa wanahitaji kupata matokeo mazuri hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita wa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga.

Simba inakumbuka kwamba Septemba 25 ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na bao la ushindi lilifungwa na Fiston Mayele.

SOMA NA HII  KAMATA MTONYO 'KICHELE' KUPITIA JACKPOT YA PIA NDANI YA CASINO YA MERIDIANBET...