Home Simba SC MAJERAHA YA LUKOSA YAMFANYA GOMES ‘KUWEWESEKA’

MAJERAHA YA LUKOSA YAMFANYA GOMES ‘KUWEWESEKA’


NAELEZWA kuwa kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa hajavutiwa na mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Junior Lukosa kutokana na madai ya majeruhi yaliomuweka nje kwa muda mrefu akiwa na klabu ya Esparance ya Tunisia.

Lokosa amejiunga na Simba kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuachana na Esparance lakini hadi sasa hajaweza kucheza mchezo wowote wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatano, limezipata kutoka ndani ya benchi la ufundi wa timu hiyo kuwa kocha huyo hajavutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo raia wa Nigeria kutokana na kukosa rekodi ya kucheza mechi nyingi katika timu aliyopita kabla ya kutua Simba.

“Ukweli mwalimu wala hajavutiwa naye na ngumu kuweza kumuamini katika hii michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na rekodi yake halafu hajacheza michuano yoyote kwa kipindi kirefu.

“Kocha mwenyewe amesema ni ngumu kumuamini kumpa nafasi kwenye mechi kubwa ambazo timu itakuwa inahitaji matokeo, maana alimwita wakati alivyokuja na alimuuliza baadhi ya vitu kisha akaongea na rafiki zake wakamueleza namna alivyo hasa juu ya suala la majeraha,” alisema mtoa taarifa.

SOMA NA HII  KIPA MBRAZILI KATEMA BUNGO BWANA, AMESHAPEWA MKONO WA KWAHERI, MWAMBA HUYU HAPA SASA KUTOKA AMERIKA ATUA MSIMBAZI