Home Habari za michezo WAKATI WATU WAKIDHANI GSM NDIO KILA KITU…ENG HERSI AMTAJA ALIYEIPA MAFANIKIO YANGA…

WAKATI WATU WAKIDHANI GSM NDIO KILA KITU…ENG HERSI AMTAJA ALIYEIPA MAFANIKIO YANGA…

Habari za Yanga SC

Rais wa Klabu ya Young Africans, Eng. Hersi Ally Said amesema kuwa, mtu aliyeko nyuma ya mafanikio ya Klabu hiyo ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Al Ahly mjini Cairo, nchini Misri ambako timu yake imekwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Chachu ya mafanikio ya mpira wetu Tanzania ni Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye soka la nchi yetu.

Taifa Stars kufuzu kwenda kwenye fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast ni moja katika mafanikio yake.

Kufaulu kwa UMOJA BID katika kuandaa AFCON 2027 ni sehemu kubwa ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha mchango wake mkubwa katika kujenga Hamasa kupitia “GOLI LA MAMA” umeifikisha Young Africans katika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23 na sasa Young Africans kufuzu kwenda robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika.

Asante Sana Mama” Amesema Rais wa Young Africans Eng.Hersi Ally Said kwenye Kituo cha Televisheni cha @alahlytv Cairo, Egypt

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE: PABLO NI SHABIKI WA MADRID ALIYEDANGANYA ALIKUWA MSAIDIZI WA ZIDANE...ALIJUA ATAFUKUZWA TU...