Home Simba SC MSHAMBULIAJI NAMBA MOJA KMC AOMBA KURUDI SIMBA

MSHAMBULIAJI NAMBA MOJA KMC AOMBA KURUDI SIMBA


MSHAMBULIAJI Charles Ilnfya ambaye alipelekwa kwa mkopo ndani ya KMC ili akuze kiwango chake, amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kurudi Simba ili kuendelea pale alipoishia.


Nyota huyo ambaye alipewa dili la miaka 
miwili ndani ya Simba, alikwama kufurukuta zama za Sven Vandenbroeck na alitolewa kwa mkopo kurudi kwenye timu yake ya zamani KMC ambapo huko aliweza kutupia mabao sita na pasi mbili za mabao.

 

SOMA PIABAADA YA MANARA ‘KUMTAPIKIA NYONGO’..BARBARA AMJIBU HIVI ‘KIBABE’


Akizungumza na Championi Jumamosi, Ilanfya alisema kuwa kwa sasa anafikiria kurudi Simba kwa kuwa uwezo anao na anatambua kwamba uwezo wake ni mkubwa.

 

“Nilipokuwa ndani ya KMC nilikuwa ninawasiliana na viongozi kutoka Simba ambapo walikuwa wananifuatilia pia jambo ambalo lilifanya niongeze juhudi.

 

“Kwa hapa ambapo nipo ninaweza kusema kwamba uwezo wa kucheza Simba upo na ninaweza hivyo ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuaje,” alisema Ilanfya.

SOMA NA HII  MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA...SIMBA WAPEWA WYDAD..YANGA vs AL AHLY...