Home kimataifa GREALISH AVUNJA REKODI YA USAJILI

GREALISH AVUNJA REKODI YA USAJILI


USAJILI wa nyota wa Aston Villa ndani ya kikosi cha Manchester City , Jack Grealish ambaye amepewa dili la miaka sita akitokea kikosi cha Aston Villa  umevunja rekodi ya dau la Paul Pogba wa Manchester United aliloweka mwaka 2016 katika rekodi za uhamisho nchini Uingereza.

Manchester City wamemsainisha Grealish mwenye miaka 25 kwa dau la pauni milioni 100 ikiwa ni dili kubwa kufanyika katika masuala ya soka hasa katika timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England na ni jana aliweza kufanyiwa vipimo na kusaini dli hilo.

Rekodi ya Paul Pogba wakati anajiunga na Manchester United ambayo ilikuwa inaishi ilikuwa ni dau la pauni milioni 93.25 na alikuwa akitokea Klabu ya Juventus 2016.

Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola alikuwa kwenye mpango wa muda mrefu kuhitaji saini ya nyota huyo ambaye amecheza jumla ya mechi 213 na amefunga mabao 32 katika misimu nane.

Pia amepewa jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na nyota Sergio Aguero ambaye kwa sasa ameibukia ndani ya kikosi cha Barcelona.

SOMA NA HII  OLE GUNNAR KUPEWA MKATABA MPYA KUINOA TIMU HIYO