Home Habari za michezo SIKU MOJA BAADA YA KUPEWA ‘THANK YOU’….KONKONI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA ALICHOTAKA YANGA….

SIKU MOJA BAADA YA KUPEWA ‘THANK YOU’….KONKONI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA ALICHOTAKA YANGA….

Habari za Yanga

Straika Hafiz Konkoni amekiri kufikia makubaliano na Yanga kutolewa kwa mkopo, ambapo kwa sasa amesisitiza anahitaji kwenda nyumbani kwao Ghana, akapumzishe akili yake kidogo.

Amesema atakwenda kucheza soka la kulipwa nchini Cyprus ambako atacheza miezi minne pekee, ingawa hakutaja ni timu gani.

“Sikutaka kuondoka Yanga, ila kwa usalama wa karia yangu imenibidi nifanye maamuzi hayo, nje na hapo ningelazimika kusubiri hadi dirisha kubwa,” amesema na kuongeza;

“Nimepokea ofa nyingi sana kama kutoka Romani na nchi mbalimbali na jambo la msingi zaidi, nitahitaji Yanga inilipe pesa yangu yote ya usajili,”

“Natarajia kuondoka kwenda nyumbani nikapunguze ‘stress’ zilikuwa nyingi sana, baada ya hapo mambo mengine yataendelea,” amesema

DATA ZAKE

Amecheza jumla ya dakika 189 dhidi ya KMC (dakika 26), JKT Tanzania (59), Geita Gold (31), Azam (dakika moja) na Singida Fountain Gate (dakika 72), amefunga bao moja na asisti moja dhidi ya KMC.

SOMA NA HII  SIKU 100 TOKA AAJIRIWE SIMBA...HIVI NDIVYO AHMED ALLY ALIVYOJITOFAUTISHA NA MANARA...