Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUMALIZANA NA WAARABU LEO…MWAMNYETO ATOA HOFU YANGA….

SAA CHACHE KABLA YA KUMALIZANA NA WAARABU LEO…MWAMNYETO ATOA HOFU YANGA….

Habari za Yanga leo

Nahodha na beki wa kati wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amewaambia Wanayanga waondoe hofu, kwani wapo Algeria kulipa kisasi cha kuwafunga na MS Algers sambamba na kubeba Kombe la Shirikisho Afrika.

leo Juni 3, , timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa mkondo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa nchini Algeria.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga ilifungwa mabao 1-2, hivyo inahitaji kupata ushindi wenye wastani wa mabao 2-0 ili kubeba ubingwa.

Akizungumza nasi, Mwamnyeto alisema anaamini mchezo utakuwa mgumu, lakini hiyo haiwafanyi waingie kinyonge, zaidi watapambana kupata ushindi mkubwa wa mabao.

Mwamnyeto alisema maandalizi waliyoyafanya yanatosha kabisa, wao kupata ushindi na kuandika historia ya kubeba kombe hilo.

Aliongeza kuwa, morali ya wachezaji ipo kubwa kambini na kila mmoja ameahidi kupambana kufa au kupona ili kupata ushindi.

“Kama wao walitufunga nyumbani, basi sisi hatushindwi kuwafunga hapa kwao.

“Kocha ameangalia upungufu na ubora wa wapinzani wetu wanapokuwa wanacheza mechi za nyumbani, hivyo tunaamini tutafanya vizuri,” alisema Mwamnyeto.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa: “Tunakwenda ugenini baada ya wao kupata ushindi kwetu, tunaamini tumekuwa tukifanya vizuri kwenye mechi za ugenii, hilo linatupa nguvu ya kuamini kwamba tutafanya vizuri.”

Naye mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele ambaye ni kinara wa mabao Kombe la Shirikisho Afrika akiwa nayo saba, amesema kwamba: “Tunafahamu huu ni mchezo ugumu kwa kuwa ni fainali na tunacheza dhidi ya timu ngumu ambayo imepata ushindi ugenini.

“Lakini kama timu tayari tumesahau matokeo ya mchezo uliopita na tupo tayari kupambana kushinda mchezo huu wa ugenini, tunachoomba ni mashabiki wetu kuendelea kutuombea kheri tuwe salama mpaka siku ya mchezo.”

REKODI YA YANGA SHIRIKISHO UGENINI
US Monastir 2-0 Yanga
Real Bamako 1-1 Yanga
TP Mazembe 0-1 Yanga
Rivers Utd 0-2 Yanga
Marumo 1-2Yanga.

SOMA NA HII  MKANDA MZIMA WA SAKATA LA MWAKINYO HUU HAPA....ISHU YA KUMGOMBEA DEMU YATAJWA...