Home Habari za michezo KATI YA HAWA MMOJA KUMRITHI CHAMA SIMBA….BENCHIKHA KAPITISHA USAJILI WA HUYU KWANZA…

KATI YA HAWA MMOJA KUMRITHI CHAMA SIMBA….BENCHIKHA KAPITISHA USAJILI WA HUYU KWANZA…

Tetesi za usajili Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha, amewasilisha jina la kiungo wa zamani wa Paide Linnameeskond nchini Estonia, Babou Cham raia wa Gambia kwa ajili ya kuwa mbadala wa Clatous Chama.

Benchikha tayari amewasilisha orodha ya wachezaji anaowahitaj kwa ajili ya kuongezwa katika dirisha dogo kati ya hao, yupo kiungo mkabaji Babacar Sarr aliyetambulishwa mwishoni mwa juma lililopita.

Kocha huyo anaendelea kukiboresha kikosi chake kwa kuongeza maingizo mapya katika dirisha dogo, kati ya hao amebakisha mshambuliaji pekee baada ya kumpata kiungo mkabaji na huyo mshambuliaji ambaye amependekeza asajiliwe.

Kwa mujibu wa taarifa Kutoka ndani ya Klabu hiyo ya Msimbazi, licha ya ugumu wanaoupata SimbaSC wa kuipata saini ya kiungo huyo mwenye uwezo wa kutokea kulia na kushoto, lakini uongozi wa klabu hiyo umeahidi kupambana kuipata saini ya nyota huyo.

Mtoa taarifa huyo amesema dili hilo lipo katika hatua za mwisho kukamilika, kutokana na mazungumzo yanayoendelea kati ya menejimenti ya mchezaji huyo na Uongozi wa Simba SC.

Ameongeza kuwa, kiungo huyo anakuja kuchukua nafasi ya Chama ambaye, inaelezwa Kocha Benchikha amemuondoa katika mipango yake ya msimu huu kwa kile kilichotajwa utovu wa nidhamu.

“Asilimia kubwa ya wachezaji ambao wametambulishwa baada ya usajili wao kukamilika katika dirisha dogo, wote ni mapendekezo ya Kocha Benchikha ambaye aliwasilisha majina yao.

Kati ya hao yupo kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wa kutokea kulia na kushoto raia wa Gambia, anaitwa Babeu Cham, jina lake limependekezwa na kocha ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Chama.

“Chama ni kati ya wachezaji ambao kocha amewaondoa katika mipango yake, hivyo kama taratibu zikikamilika basi tutamsajili katika dirisha hili dogo,” amesema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema: “Usajili uliokamilika ndiyo tunauweka wazi, kwa sasa jina la huyo kiungo mpya bado halijafika mezani kwangu, lakini kikubwa ifahamike kuwa suala la usajili lote lipo chini ya kocha ambaye viongozi hatutamuingilia.”

Rekodi zinaonesha kwamba, nyota huyo kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Paide kumalizika, huku akiwa amewahi kucheza Nomme United ya Estonia, Ararat Yerevan (Armenia), SC Noravank (Armenia), FC Sevan (Armenia) na Real de Banjul ya kwao Gambia.

SOMA NA HII  MANARA AMWAGIA SIFA HIVI NGOMA