Home Habari za michezo ENG HERSI AFUNGUKA SIRI YA USAJILI YANGA….AANIKA ALIVYOMNYAKUA AZIZI KI KININJA…

ENG HERSI AFUNGUKA SIRI YA USAJILI YANGA….AANIKA ALIVYOMNYAKUA AZIZI KI KININJA…

Tetesi za Usajili Yanga

Rais wa Yanga, Hersi Said amesema siri ya kusajili wahezaji bora kipindi cha hivi karibuni akikiri kuwa ni mchakato na kutambua upungufu wa timu kabla ya usajili.

“Kugundua upungufu, baada ya hapo kutafuta mtu ambaye anaweza kuziba pengo na kuongeza thamani ya ubora wa eneo hilo na ni mtu wa aina gani,” amesema.

“Baada ya hapo kutafuta muunganiko kwa kushirikisha benchi la ufundi, ambaye atataka kujua namna ya kumfuatilia mchezaji huyo ili kujua aina ya uchezaji wake, umri wake na urefu wake,” amesema Hersi kwenye moja ya mahojiano na kituo cha Clouds Media.

Hersi amesema baada ya hayo yote pia amekuwa akiangalia kiwango cha mchezaji anayetaka kumsajili kwa wakati husika ikiwa ni pamoja na kuangalia taarifa zake na majeraha.

Amesema baada ya kufuatilia hayo kazi inayofuata ni namna ya kumshawishi mchezaji huyo ili aweze kukubali ofa ya kucheza Yanga huku akikiri kuwa ushawishi unaingia hadi kwenye fimilia na mahusiano, akitoa mfano namna walivyonasa saini ya Aziz KI baada ya mama mzazi wa mchezaji huyo kuongeza ushawishi kwa mwanaye.

SOMA NA HII  BOCCO MAMBO SIO MAMBO SIMBA,MGUU NJE MGUU NDANI.... ISHU KAMILI IKO HIVI