Home Habari za michezo KISA MECHI YA JANA….MORRISON AMTIA NGUMI ZA USO SHABIKI WA YANGA….AFIKISHWA POLISI...

KISA MECHI YA JANA….MORRISON AMTIA NGUMI ZA USO SHABIKI WA YANGA….AFIKISHWA POLISI CHAP…


Muda mfupi baada ya kumalizika mchezo wa Yanga dhidi ya Simba mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison amefikishwa kituo cha Polisi kwa madai ya kumshambulia mtu.

Taarifa zinaeleza kwamba tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mchezo wa ‘Kariakoo Derb’.

 Morrison amehojiwa katika kituo cha Polisi Chang’ombe  kutokana na shambulio hilo dhidi ya shabiki wa Yanga.

Mmoja wa maofisa wa Polisi ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema shabiki huyo inadaiwa alimdhihaki Morrison kwa kumuita mwizi wa gari ndipo baadhi ya mashabiki wa Simba na mchezaji huyo raia wa Ghana kumshambulia kisha kumwacha na majeraha mwilini.

Tukio hilo limetokea wakati mshambuliaji huyo akitaka kuondoka uwanjani baada ya mchezo huo ambao umemalizika kwa suluhu.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA NA GSM WAKITAKA KUMPA MIL 400 ...HIVI NDIVYO MO DEWJI ALIVYOFANYA KUFURU ISHU YA CHAMA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here