Home Habari za michezo BOCCO MAMBO SIO MAMBO SIMBA,MGUU NJE MGUU NDANI…. ISHU KAMILI IKO HIVI

BOCCO MAMBO SIO MAMBO SIMBA,MGUU NJE MGUU NDANI…. ISHU KAMILI IKO HIVI

Habari za Simba SC

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru (Free agent) ambapo hakuna mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.

Kapteni John Bocco inatajwa hayupo kabisa kwenye mipango ya klabu ya Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Mpaka hivi sasa tayari klabu imempa taarifa kuwa itaachana nae hivi karibuni.

Simba inamtazama John Bocco kuwa miongoni mwa washauri wa timu hiyo baada ya mkataba wake wa utumishi kwa Wekundu wa Msimbazi kumalizika,

Simba inasubiri ripoti ya Bocco mwishoni mwa mwezi ujao kama atakubali wadhifa huo ama laaah.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI

1 COMMENT