Home Habari za michezo AL AHLY KUTUA DAR LEO, MASTAA HAWA WA YANGA NJE YA DIMBA

AL AHLY KUTUA DAR LEO, MASTAA HAWA WA YANGA NJE YA DIMBA

Habari za Michezo leo

Ofisa Habari na mawasiliano wa Al Ahly, Gamal Gabr amesema timu hiyo itatua nchini leo na wachezaji 25 huku nyota watatu Taher Mohamed, Antony Modeste na Mahmoud Metwaly wakiwa kwenye hatihati ya kuukosa mchezo dhidi ya Yanga wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hizo zilizopo Kundi D zinakutana katika mchezo huo utakaopigwa saa 1:00 usiku huku Al Ahly ikitoka suluhu katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Smouha na kufikisha pointi 14 nyuma ya vinara Pyramids yenye pointi 16.

Yanga inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kundi hilo kwani baada ya hapo itakwenda Ghana.

SOMA NA HII  SIMBA DAY YAWANG'ARISHA MASTAA HAWA

2 COMMENTS