Home Azam FC MASTAA AZAM FC WAMUAMULIA KOCHA WAO…WAPANGA KUMFANYIA ‘NDOMBOLO’…AFUKUZWE..

MASTAA AZAM FC WAMUAMULIA KOCHA WAO…WAPANGA KUMFANYIA ‘NDOMBOLO’…AFUKUZWE..

Habari za Azam

Hatimaye Jinamizi la Makocha kukataliwa na wachezaji wa Azam limeibuka tena na sasa ni kwa kocha Dabo.

Habari za Uhakika ni kwamba safari hii ni zamu ya Yousouph Dabo, Taarifa zinasema kuwa Mkasa wa Dabo ulianza siku ya mazoezi kwanza baada ya mechi ya Yanga, Baada ya kichapo, Dabo aliwakosoa wachezaji wake mazoeziniakiwalaaumu kwa kucheza chini ya kiwango na hawakufuata maelekezo yake.

Akaenda mbali akawaambia wachezaji wasijione wako salama, atamuondoa mchezaji yoyote ambaye hatafuta malekezo yake kwenye disrisha dogo la usajili.

Chanzo chetu kinasema kauli hii iliwakera sana wachezaji, na kuanzia hapo walikubaliana kwamba wafanye wanavyoweza kufanya ili kocha huyo afukuzwe.

Chanzo chetu kinaendelea kutujulisha kwamba kabla ya mchezo wao na Namungo wakati wachezaji wakipasha moto misuli Dabo aliwaambia wachezaji wake kwamba watapoteza mchezo kwasababu hawakuonyesha kama wako tayari kwa mchezo huo.

Na kama ambavyo kila mtu aliona ndivyo hali ilivyokuwa, Azam ililala kwa kipigo cha goli 3-1 huku timu ikicheza kwa ari ya chini sana.

Na kwa taarifa za ndani ni kwamba wachezaji wamepanga kundelea na kumuhujumu Dabo kwenye michezo ijayo hadi afukuzwe, Ikumbukwe Azam leo anacheza na Mashujaa kigoma

Wachezaji wa Azam wanalalamika kwamba Kocha Dobo ni Mkali sana na hataki kusikia ushauri wa yoyote ndani ya timu, Wacheaji wa Azam wamekuwa na Malalamiko kwa kocha huyo muda mrefu sasa.

Hivi baada ya Azam kutolewa kwenye Mashindano ya kimataifa ya Shirikishao CAF, Mchambuzi mmoja wa mmoja wa wawachezaji wa Azam aliandika juu ya hali isivyoshwari kwnye chumba cha kuvalia wachezaji, inaonekana mchambuzi huyo alijulishwa na mchezaji wake mkasa huo.

Hata hivyo taarifa zinatanabaisha kwamba pamoja na msuguano huo wamiliki wa Azam FC wamesema wamechoka kufukuza makocha kila mwaka huku mambo yakishindwa kubadilika, safari hii wameamua kuziba masiko juu ya malalamiko ya wachezaji kama itabidi kufukuzwa basi wafukuzwe wachezaji lakini sio kocha.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAKE WAPYA, ROBERTINHO AWAPIGA MKWARA MZITO YANGA