Home Habari za michezo TAIFA STARS, YANGA KUWANIA TUZO ZA CAF MSIMU HUU…..SIMBA ‘WABANIWA’….

TAIFA STARS, YANGA KUWANIA TUZO ZA CAF MSIMU HUU…..SIMBA ‘WABANIWA’….

Habari za Michezo

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza Timu za Taifa, Vilabu na Wachezaji wanaowania tuzo hizo mwaka 2023 ambapo Taifa Stars ya Tanzania itachuana na Timu za Taifa za Cape Verde, Gambia, Guinea Bissau, Equatorial Guinea, Mauritania, Morocco, Msumbiji, Namibia na Senegal.

Kwa upande wa Vilabu, Mabingwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga Africans inashindana na CR Belouizdad, USM Alger, ASEC Mimosas, AL Ahly FC, Raja CA, Wyadad AC, Mamelodi Sundowns, Marumo Gallants, na ES Tunis.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Desemba 11, 2023 Nchini Morocco, zimeiacha nje ya kinyang’anyiro Klabu ya Simba kutoka Tanzania.

SOMA NA HII  GAMONDI ATUMIA DAKIKA 180 KUWASOMA SIMBA