Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUTEMWA NA SIMBA…PABLO AIBUKA NA HILI KUHUSU KIBU...

SIKU CHACHE BAADA YA KUTEMWA NA SIMBA…PABLO AIBUKA NA HILI KUHUSU KIBU NA SAKHO…ATAKA KURUDI TENA BONGO..


SIKU chache tangu aachane na Simba, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pablo Franco amefichua ndani ya kikosi hicho kimejaa mafundi, lakini alikunwa zaidi na washambuliaji, Pape Ousmane Sakho na Kibu Denis, alisema kama watabaki kikosini wataibeba zaidi timu hiyo msimu ujao.

Sakho amemaliza msimu akiwa na mabao sita na kuasisti sita, huku Kibu akiwa kinara na mabao nane na asisti nne, wakiwa ndio wachezaji waliohusika na mabao mengi ya timu hiyo kwa msimu huu, wakichangia mabao 24 kati ya 41 yaliyofungwa na timu hiyo.

Akizungumza  kutoka Hispania, Pablo alisema Kibu na Sakho walikuwa kivutio kikubwa kwake kwa muda wote aliofundisha nchini, japo aliwapongeza wachezaji wote kwa mchango walioutoa akiwa nao.

“Wakati nakuja Kibu (Denis) alikuwa katika kiwango bora, ila Sakho alipata majeraha. Alirejea taratibu na kadri alivyoanza kucheza alitoa msaada mkubwa katika timu hivyo kwangu ni wote wawili najivunia,” alisema Pablo na kuongeza;

“Nawatabiria makubwa sana kwa ustawi wa Simba na Tanzania, ni nchi ya kipekee niliyofurahia kufanya kazi pamoja na familia yangu, nina imani ipo siku nitarejea tena.”

Pablo aliifundisha Simba tangu Nov 10, 2021 hadi Mei 31, mwaka huu.

Kauli ya Pablo iliungwa mkono na msaidizi wake, Seleman Matola alisema anafurahishwa na kujitoa kwa wachezaji, huku akiwamwagia sifa nyota hao kwa kiwango chao.

SOMA NA HII  KUHUSU TIMU GANI ATAICHEZEA MSIMU UJAO...DILUNGA AIKANA SIMBA...AIITA YANGA MEZANI...