Home Habari za michezo KUHUSU TIMU GANI ATAICHEZEA MSIMU UJAO…DILUNGA AIKANA SIMBA…AIITA YANGA MEZANI…

KUHUSU TIMU GANI ATAICHEZEA MSIMU UJAO…DILUNGA AIKANA SIMBA…AIITA YANGA MEZANI…

Dilunga akiwa Simba SC

Kiungo wa zamani wa Simba SC, Hassan Dilunga amesema msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara yupo tayari kucheza timu yoyote ikiwemo Yanga lakini kipaumbele chake cha kwanza ni maslahi.

Dilunga amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuumia wakati akiitumikia Simba SC.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na JKT Tanzania amesema; “Nipo tayari kucheza popote kikubwa maslahi, atakaekuja vizuri na tukaelewana nae ndiko nitakapocheza.”

Kuhusu kurudi Simba SC amesema; “Naendelea kuwasikilizia nafanya nao tu mazoezi kama ambayo ninavyofanya na Mtibwa na timu zingine.”

Hata hivyo Mchezaji huyo ameushukuru uongozi wa Simba SC kwa kumtibu kwa ufasaha kipindi alichokuwa akiumwa.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru viongozi wa Simba wamenipambania kuhakikisha napata tiba sahihi, nimepata nawashukuru nimepona kwa asilimia 100,” amesema Dilunga

SOMA NA HII  NDAYIRAGIJE KOCHA MKUU GEITA GOLD