Home Habari za michezo YANGA WAANIKA SABABU ZA KUTOKUWA NA GWARIDE LA UBINGWA WA ASFC ….GSM...

YANGA WAANIKA SABABU ZA KUTOKUWA NA GWARIDE LA UBINGWA WA ASFC ….GSM APATWA NA MSIBA MKUBWA…


Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema timu hiyo haitafanya gwaride kama ilivyofanya wakati ilipochukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo kupitia Manara ilieleza kusitisha zoezi hilo wakati timu itakapotua Jijini Dar es Salaam saa 12 za jioni ikitokea Arusha ilipofanyika fainali hiyo dhidi ya Coastal Union.

Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya kumalizika kwa kufungana mabao 3-3 ndani ya dakika 120 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Manara amesema baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere wachezaji watapanda moja kwa moja kwenye basi la timu na kwenda Makao Makuu ya Klabu hiyo kwa ajili ya kulikabidhi Kombe kwa viongozi na wazee.

Amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika Makao Makuu ya Klabu yao yaliyokuwa mtaa wa Twiga na Jangwani ili kujumuika kwa pamoja katika mafanikio hayo muhimu kwao msimu huu.

Katika hatua nyingine Manara ametoa salamu za pole kwa Mmiliki wa timu hiyo, Ghalib Said Mohamed (GSM) kufuatia kufiwa na kaka yake wa kuzaliwa naye Mama na Baba mmoja aliyefariki jana huko Mumbai India baada ya kusumbuliwa na Moyo.

Manara amewataka mashabiki na wanachama kuendelea kusubiri taarifa rasmi ya kuwasili kwa mwili huo na taratibu za mazishi.

SOMA NA HII  KISA KUSUGULISHWA BENCHI...BIGIRIMANA AVUNJA UKIMYA YANGA...ADAI YEYE NI BORA...