Home Yanga SC YANGA YAFUNGA MZUNGUKO WA PILI KWA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA

YANGA YAFUNGA MZUNGUKO WA PILI KWA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kimelazimisha sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Licha ya Yanga kupambana kusaka ushindi sawa na Dodoma Jiji ambao ni wenyeji ngoma ilikuwa nzito kwa timu zote ambapo zimegawana pointi mojamoja.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kukamilisha msimu wa 2020/21 ikiwa nafasi ya pili na pointi zake ni 74.

Dodoma Jiji inakamilisha mzunguko ikiwa nafasi ya 8 na pointi zake ni 44.

SOMA NA HII  KWENYE MEI MOSI JANA...STAILI YA MAYELE YA KUTETEMA YAPIGWA MBELE YA RAIS SAMIA...WATU WAPAGAWA..