Home Uncategorized BREAKING: ZAHERA AFUNGIWA MECHI TATU KUITUMIKIA YANGA

BREAKING: ZAHERA AFUNGIWA MECHI TATU KUITUMIKIA YANGA


Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufuatao:

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YAITUNGUA BAO 1-0 NAMUNGO, MAJALIWA