Home Uncategorized YANGA V SIMBA, HUYU ANASHIIKILIA REKODI YA KUWATUNGUA WAPINZANI WAO MACHI 8,...

YANGA V SIMBA, HUYU ANASHIIKILIA REKODI YA KUWATUNGUA WAPINZANI WAO MACHI 8, KESHO SWALI LITAJIBIWA


KESHO Machi 8 2020, Uwanja wa Taifa,Simba itakuwa ugenini ikicheza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.
Simba ipo chini ya Mbelgiji Sven Vandenbroeck huku Yanga ikiwa chini ya Luc Eymael ambaye naye pia ni raia wa Ublgiji.
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa mwaka 2014/15 kwenye mchezo wa watani wa jadi uliochezwa Machi 8 mabingwa watetezi walikuwa nyumabani na waliikaribisha Yanga.
Simba ilishinda mchezo huo kwa bao 1-0 lililofungwa na Emannuel Okwi dakika ya 52
Kesho saa 1:00 Yanga itakuwa nyumbani ikiikaribisha Simba na itakuwa Machi 8 swali kubwa litajibiwa kesho ambapo kila timu imejipanga kupata ushindi.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa msimu huu Simba ikiwa mwenyeji ilishuhudia Yanga ikipindua meza kibabe na kuufanya ubao kusoma 2-2.

Simba ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao moja lililofungwa na Medie Kagere na kipindi cha pili waliongeza bao la pili kupitia kwa Deo Kanda.

Kwa upande wa Yanga meza ilipinduliwa na Mapinduzi Balama pamoja na Mohamed Issa.
SOMA NA HII  YANGA HAO KUIFUATA KAGERA SUGAR