Home Burudani BAADA YA KUISHIKA BONGO…MANDONGA AHAMISHIA MAJESHI KENYA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

BAADA YA KUISHIKA BONGO…MANDONGA AHAMISHIA MAJESHI KENYA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Mandonga

Karim ‘Mandonga’ Said ni kama amepewa bondia wa levo yake, nchini Kenya atakapopanda ulingoni Januari 14 kuzichapa pambano lisilo la ubingwa la uzani wa middle.

Mandonga atazichapa Denzel Onyango Okoth, jijini Nairobi, ikiwa ni pambano lake la kwanza la kimataifa tangu alipoingia kwenye masumbwi 2018.

Bondia huyo mwenye tambo, ni kama amepewa bondia ‘saizi’ yake kwenye ubora, wote wakiwa na nyota moja ingawa mpinzani wake hajawahi kupigwa.

Hata hivyo, Mkenya huyo bado ni chipukizi kwenye ndondi za kulipwa akiwa amepigana mapambano mawili pekee na kushinda yote kwa Technical Knock Out (TKO).

Pambano la kwanza alimchapa Denis Otieno raundi ya pili Machi 5, 2022 na miezi saba baadae alimchapa Mussa Omar Nassor raundi ya kwanza.

Mandonga ambaye hivi karibuni ametoka kushinda kwa TKO na kushtua tasnia ya ngumi nchini alipomchapa Said Mbelwa, anasema hivi sasa kiwango kimepanda na anakweda Kenya na staili mpya ya ndondi.

“Naipeleka ngumi ya Ukraine, Kenya, mpinzani wangu ajipange kweli kweli,” alijinasibu bondia huyo anayekamata nafasi ya 5 nchini kwenye uzani wake mwenye rekodi ya kushinda mara tatu, amepigwa mara tatu na kutoka sare mara moja tangu 2018.

SOMA NA HII  KUHUSU KIWANGO WA DIARRA SIKU HIZI .....MBRAZILI YANGA AANIKA MBIVU NA MBICHI ZOTE....MSHERI ATAJWA....