Home Habari za michezo MANARA AMWAGIA SIFA HIVI NGOMA

MANARA AMWAGIA SIFA HIVI NGOMA

Habari za Simba

Aliyekuwa Afisa Mhamasishaji wa Yanga,Haji Manara amesema kuwa Kocha Robertinho Oliveira alikua anakosea kumpanga Fabrice Ngoma katika eneo la kiungo cha ukabaji wakati kwa uhalisia Midifield Teacher ni kiungo ambaye uwezo wake ni kuchezesha timu na si mtu wa kazi chafu.

Manara amemtaja Ngoma kuwa ni fundi kweli wa mpira,na huwa anaonekana zaidi pale timu inavyoshambulia,inao mpira,lakini Simba inapokutana na timu kama ya Yanga,Ngoma anaonekana dhaifu!

Amesema Ngoma alipokutana na Khalid Aucho na Mudathir Yahya ambao kiasili ni wakabaji,wakatili na hawatoi nafasi ya kufanya jambo lako kiurahisi,lazima aonekane wa kawaida ikizingatiwa anachezeshwa katika eneo lisilo lake.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA ACHENI CHUKI...MNAPASWA KUMUOMBA RADHI KIBU DENNIS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here