Home Habari za michezo SIMBA, TP MAZEMBE WAPEWA ONYO SAUZI…… ISHU KAMILI IKO HIVI

SIMBA, TP MAZEMBE WAPEWA ONYO SAUZI…… ISHU KAMILI IKO HIVI

Tetesi za Usajili Simba

Klabu ya Richards Bay inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini (Dstv Premiership) imezionya Klabu za Simba na TP Mazembe kuacha kumshawishi golikipa wao, Salim Magoola, Raia wa Uganda ili atie kandarasi ya kuzichezea kwa njia zisizo sahihi

Magoola ni miongoni mwa magolikipa wanaofanya vyema pale PSL ambapo Simba Sc na ndugu zao TP Mazembe wameamua kwenda moja jwa moja kwa mchezaji huyo kumshawishi ili wapate saini yake .

Richards Bay hawajavutiwa na kitendo hiki kwa sababu wao ndiyo wamiliki halali wa mchezaji huyo ambaye mtakaba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu lakini kuna kipengere cha kumwongeza mwaka mmoja.

Simba Sc bado wanasaka golikipa mwingine na magoola ni moja ya walinda mlango wa kiwango cha juu hapa Afrika wakati huu.

Mwandishi wa Idisk Times Lorenzo Kohler ameripoti habari hii.

SOMA NA HII  LIVERPOOL YABAMIZA MTU MKONO