Home Habari za michezo HIVI NDIVYO WAGUINEA WALIVYOIPOKEA SIMBA KWAO…HOROYA TUMBO JOTO…

HIVI NDIVYO WAGUINEA WALIVYOIPOKEA SIMBA KWAO…HOROYA TUMBO JOTO…

Habari za Simba SC

Mratibu wa Klabu ya Simba SC Abbas Ally amesema hali ya hewa ya mjini Conakry, Guinea haina tofauti sana na nyumbani Tanzania, na pia watu Guinea wanaizungumza Simba SC, kwa maana wanaifahamu japo haijawahi kucheza nchini humo.

Simba SC itapapatuana na Horoya AC katika mchezo wa Kwanza wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrrika Jumamosi (Februari 11), katika Uwanja wa General Lansana Conte, majira ya saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

Abbas ambaye ametangulia nchini Guinea kwa ajili ya kuweka mambo sawa kabla ya kikosi cha Simba SC kuwasili baadae leo Alhamis (Februari 09), amesema tangu amefika mjini Conakry, hali ya hewa ya hapo ipo vizuri na haina tofauti kubwa na jijini Dar es salaam.

Amesema kwa mazingira hayo anaamini kikosi chao kitakua na wakati mzuri wa kujiandaa kabla ya kuingia kwenye mchezo siku ya Jumamosi, huku wakiamini kupata matokeo chanya.

“Hali ya hewa hapa ipo vizuri sana, haina tofauti kubwa na nyumbani Dar es salaam, kwa mazingira haya ninaamini wachezaji watakua wakati mzuri wa kujiandaa kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Horoya AC Jumamosi,”

“Kuhusu Simba SC hapa Conakry, imekuwa ikitajwa sana na baadhi ya wananchi wa hapa, wanaitaja kwa mazuri kwa sababu imekuwa sehemu ya timu zinazofanya vizuri kimataifa kwa miaka ya karibuni, hii inaonesha timu yetu inaendelea kujitangaza kila kona ya Afrika na kwingineko.” amesema Abbas Ally

Kikosi cha Simba SC kimeondoka jijini Dar es salaam mapema leo Alhamis majira ya Alfajiri, kuelekea Counakry kupitia mjini Addis Ababa Ethiopia.

SOMA NA HII  MO AWAPIGIA SIMU WACHEZAJI WOTE SIMBA SC