Home Habari za michezo MAYELE AONYESHA ‘MAHABA’ YA WAZI KWA MASTAA WA SIMBA…AWAITA KWENYE KIKOSI CHAKE...

MAYELE AONYESHA ‘MAHABA’ YA WAZI KWA MASTAA WA SIMBA…AWAITA KWENYE KIKOSI CHAKE BORA CHA MSIMU…


Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Fiston Kalala Mayele amesema msimu uliopita ulikuwa mguu kwao licha ya kuchukua mataji matatu huku yeye akifanikiwa kuwa mfungaji bora wa Yanga na mfungaji wa pili wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 16.

Akizungumzia kuhusu msimu huo, Mayele amesema mechi ngumu ilikuwa ni kati ya Yanga na Azam kwani aliumia mazoezini siku mbili kabla ya mechi lakini alisema lazima acheze na afunge kwani ilikuwa mechi mhimu kwao ili kuendelea kuwahakikishia kunyakua ubingwa jambo ambalo alifanikiwa kufunga.

Aidha, Mayele amesema kuwa mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho kati yao na Coastal Union iliwavuruga baada ya kufungwa bao la tatu, lakini bahati nzuri Mungu alikuwa upande wao na kufanikiwa kusawadhisha dakika za mwisho za nyongeza na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mikwaju ya penati.

Kikosi bora cha Fiston Kalala Mayele msimu wa 2021/2022 alichokitaja Mayele;

1. Djigui Diarra

2. Djuma Shaban

3. Mohammed Hussein ‘Tshabalala’

4. Henock Inonga Baka

5. Bakary Nondo Mwamnyeto

6. Yanick Bangala

7. Pape Osumane Sakho

8. Khalid Aucho

9. Fiston Kalala Mayele

10. Feisal Salum Abdallah

11. George Mpole

Makocha; Nasredine Mohammed Nabi na Cedrick Kaze.

SOMA NA HII  MMISRI APEWA MECHI YA YANGA vs MAMELOD....'DATA' ZOTE HIZI HAPA...