Home Uncategorized KMC WAIPA AZAM FC KOCHA

KMC WAIPA AZAM FC KOCHA


UONGO ZI wa wa timu yamanispaa ya Kinondoni, KMC umesema kuwa hauna tatizo na kocha Etienne Ndayiragije iwapo atahitaji kuondoka kwani ni maisha ya soka yalivyo.

Imeelezwa kuwa Ndayiragije tayari amenaswa na uongozi wa Azam FC kwa ajili ya kubeba mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu Hans Pluijm aliyefungashiwa virago kwa kile kilichoelezwa kufanya vibaya kwenye ligi.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamini Sita amesema kwa sasa hawana mkataba na Ndayiragije ila wamekaa kuzungumza naye ili kujua hatma yake itakuaje.

“Tunatambua kwamba Ndayiragije ni mwalimu mzuri, tumemaliza naye mkataba sasa kwa sasa, tupo naye tunazungumza juu ya kuongeza mkataba kwa kumpa mapendekezo yetu kama ataona ni ngumu ni ruksa kwenda anapopataka.

“Kuiongoza timu kuwa nafasi ya nne sio kitu chepesi na kwa sasa tumepata nafasi ya kushiriki kimataifa hivyo tunapaswa tuwe makini kwenye usajili wetu, tunajua kwamba amekuwa akihusishwa kwenda Azam FC sisi hatuna tatizo naye licha ya kwamba hizo taarifa hazijawa rasmi,” amesema.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: LIGI YA MSIMU HUU NI BALAA